1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden asema Secret Service inahitaji nguvu zaidi

16 Septemba 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amesema idara ya usalama wa taifa inahitaji nguvu zaidi baada ya jaribio la mauaji dhidi ya mgombea urais wa Republican Donald Trump.

Marekani Washington | Rais Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Andrew Harnik/Getty Images

Rais wa Marekani Joe Biden amesema idara ya usalama wa ndani ya nchi hiyo inahitaji msaada zaidi. Mwito wa Biden amutowa kufuatia tukio linaloaminika lilikuwa jaribio la kumuua mgombea wa urais wa chama cha Republican Donald Trump, ambalo lilizimwa na maafisa wa usalama.

Rais huyo wa Marekani pia amesema bado hawana ripoti kamili juu ya tukio hilo la Jumapili na kwamba ameshukuru rais huyo wa zamani yuko salama. Taarifa zinasema rais wa zamani Donald Trump anatarajia kukutana na kaimu mkurugenzi wa idara ya usalama.

Viongozi kadhaa duniani walaani tukio hilo, wakiwemo rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer. Ikulu ya Urusi imesema tukio hilo ni ishara inayoonesha kwamba kampeini ya uchaguzi nchini Marekani imepamba moto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW