1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden atahadharisha mashambulizi zaidi Syria

Angela Mdungu
25 Machi 2023

Rais wa Marekani Joe Biden ametaoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi zaidi yanayowalenga wanajeshi wa Marekani walio nchini Syria

US-Präsident Joe Biden
Picha: Mario Tama/Getty Images

Biden ametoa tahadhari hiyo baada ya ndege isiyo na rubani inayoaminiwa kuwa ni ya Iran kufanya shambulio katika kituo cha matengenezo kwenye kambi ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani karibu na mji wa al-Hasakah nchini Syria.

 Kwenye mkasa huo, mkandarasi raia wa Marekani aliuwawa na watu wengine sita walijeruhiwa. Tukio hilo liliripotiwa na wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon.

Marekani ilijibu kwa kufanya mashambulizi ya kijeshi ya anga mashariki mwa Syria yaliyolenga jeshi la Mapinduzi ya Kiislamu la Iran. Kwa mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binadamu nchini Syria, hadi sasa idadi ya waliouwawa kwenye mashambulizi hayo imefikia wanajeshi 19.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW