1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Marekani kuondoka Iraq mwishioni mwa mwaka

27 Julai 2021

Rais Joe Biden wa Marekani ametangaza kwamba uhusiano wa Marekani na Iraq utaingia katika hatua mpya ambapo wanajeshi wa Marekani watasitisha operesheni zao mwishoni mwa mwaka huu.

USA I Joe Biden und Mustafa al-Kadhimi
Picha: Susan Walsh/AP/picture alliance

Hata kabla ya Rais Biden kuingia madarakani, lengo kubwa la Marekani lilikuwa kulisaidia jeshi la Iraq, si kupigana vita kwa niaba yao bali kulijengea uwezo jeshi la nchi hiyo. Na katika hatua hii pia Biden hajatangaza mara moja kupunguza idadi ya wanajeshi nchini Iraq ambao ni 2500, ikiwa ni mwaka mmoja tangu mtangulizi wake Donald Trump kaumuru kuwaondoa wanajeshi 3000 katika utangulizi wa jitihada kama hii.

Lakini pia Biden analitoa tangazo hilo baada ya uamuzi wake wa kuliondoa jeshi la Marekani kwa ukamilifu nchini Afghanistan, ikiwa ni baada ya Marekani kuanzisha mashambulizi ya kujibu mapigo ya mashambulizi ya kigaidi ya New York ya Septemba 11,2001.

Vita vya Iraq na Afghanistan ni mzigo mzito kwa jeshi la Marekani.

Mwanajeshi wa Marekani akiwa mjini BaghdadPicha: AFP/DoD/K. Tabot

Kwa pamoja vita vya Afghanistan na Iraq vimeligharibu kwa kiwango kikubwa jeshi la Marekani na kulizuia kuondoka katika maeneo hayo na hasa baada ya kuongezea kwa mvutano na China, ambo Biden mwenyewe amenukuliwa akisema kuwa ni changamoto kubwa na ya muda mrefu.

Biden anatoa kauli ya sasa ya kuhitimisha operesheni za ndani za kijeshi za Marekani pale ilipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al-Kadhemi mjini Washington. Pamoja na kwamba bado kitisho cha kundi la Dola la Kiislamu kipo na ushawishi wenye nguvu wa Iran kwa Iraq, lakini Biden amesisitiza kwamba serikali yake itasalia jukumu la kuimarisha ushirikiano wa kiusalama.

Waziri mkuu wa Iraq atoa ahadi ya kuimarisha ushirikiano na Marekani.

Kwa upande wake Kadhemi alitilia mkazo ushirikiano wao wa kimkakati. Lakini Biden pia alisisitiza kuhusu uungwaji mkono wa Marekani katika uchaguzi wa Oktoba wa Iraq, akisdema serikali ya Marekani inafanya kazi kwa karibu zaidi na yaIraq, ushirikiano wa mataifa ya Ghuba na Umoja wa Mataifa kuhakikisha uchaguzi wa haki.

Miaka 18 baada ya Marekani kuivamia Iraq na kumuondoa mtawala wa kiimla Saddam Hussein, na miaka saba ya muungano wa kijeshi uliongozwa na taifa hilo kukabiliana na Kundi la Dola la Kiislamu, ambalo lilikuwa kitisho kwa Iraq, Marekani sasa imebadili uelekeo na kulenga aina nyingine ya usaidizi.

Kwa miaka kadhaa jeshi la Marekani limekuwa na jukumu muhimu la kuunga mkono jitihada za kijeshi nchini Iraq  kusaidia kukabiliana na Kundi la Dola la Kiislamu ambalo kwa mwaka 2014 lilikuwa limetawanyika kwa kiwango kikubwa katika maeneo mengi hadi na taifa jirani la Syria.

Vyanzo AP/AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW