1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden atangaza msaada mpya wa dola bilioni 2.5 kwa Ukraine

30 Desemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza msaada zaidi wa kiusalama wa dola bilioni 2.5 kwa Ukraine leo Jumatatu wakati akitumia wiki zake za mwisho ofisini kabla ya rais mteule Donald Trump kuchukua madaraka hapo Januari.

USA Präsident Joe Biden
Rais Joe Biden anazungumza kuhusu kifo cha Rais wa zamani Jimmy Carter Jumapili, Desemba 29, 2024,Picha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa yake Biden amesema msaada huo mpya utatoa nafasi kwa Ukraine kuwa na uwezo wa kuimarisha ulinzi wake wa anga, silaha na nyenzo zingine muhimu zitakazowasiadia katika uwanja wa mapambano dhidi ya vikosi vya Urusi. Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine unakaribia miaka mitatu na hivi karibuni wanajeshi wa Korea Kaskazini wameungana na vikois vya Urusi katika mapambano dhidi ya vikosi vya Ukraine. Mpaka sasa Marekaniimetoa jumla ya dola bilioni 175 kama msaada wa jumla kwa Ukraine, lakini hakuna uhakika kama misaada itaendelea kwa kasi hiyo chini ya utawala wa Trump, ambaye anachukua nafasi ya Biden mnamo Januari 20. Trump alisema anataka kuvimaliza vita hivyo mara moja.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW