Biden atetea rekodi ya sera yake ya kigeni licha ya mizozo
14 Januari 2025Matangazo
Biden amesema kuwa maadui wa Marekani ni dhaifu zaidi kuliko walivyokuwa wakati alipoingia madarakani miaka minne iliyopita.
Wiki moja kabla ya kumkabidhi madaraka Rais mteule Donald Trump, Biden amewahutubia wanadiplomasia wa Marekani na kusifu msaada wa utawala wake kwa Ukraine na Israel.
Kiongozi huyo ameendelea kueleza kwamba Marekani inashinda kile alichokiita "mashindano ya ulimwengu" na kuwa haitashindwa na China kiuchumi kama ilivyotabiriwa.
Amesema pia Urusi na Iran zimekuwa dhaifu kwa sababu ya vita bila kuhusika moja kwa moja kwa mkono wa Marekani.
Hata hivyo, utawala wake umekosolewa kwa kuipa Israel msaada wa silaha tangu kuzuka kwa mzozo kati ya Israel na Hamas mnamo Oktoba 7, mwaka 2023.