1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden atoa msamaha wa rais kwa mwanawe Hunter

2 Desemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa msamaha wa rais kwa mwanawe Hunter Biden na hivyo kumkinga na uwezekano wa kufungwa jela kutokana na makosa ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria na kukwepa kulipa kodi.

Marekani Washington 2024 | Biden na mwanaye Hunter
Rais Joe Biden na mwanaye Hunter Biden wakipigana pambaja Julai 24, 2024 katika ikulu ya White House MarekaniPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Hunter Biden mwenye umri wa miaka 54, alikiri makosa hayo na natarajiwa kuhukumiwa wiki chache zijazo kabla rais mteule wa Marekani Donald Trump kuchukua hatamu za uongozi.

Hatua hii inamaliza gumzo la muda mrefu kuhusiana na mwanawe Biden, ambaye mwezi mmoja baada ya babake kushinda uchaguzi wa mwaka 2020, alifichua hadharani kwamba alikuwa anachunguzwa na Mahakama.

Biden wakati huo aliapa kuheshimu utawala wa sheria lakini kutokana na hatua hiyo, Rais huyo wa Marekani anayemaliza muda wake madarakani amekwenda kinyume na ahadi yake ya awali ya kutotumia nguvu zake za urais kwa manufaa ya familia yake.

Mnamo Novemba 8 baada ya ushindi wa Trump, msemaji wa ikulu ya White House Karine Jean-Pierre aliondoa uwezekano wa msamaha kwa Hunter akisema, "tumeulizwa swali hili mara kadhaa. Jawabu letu bado ni lile lile, hapana."

Rais mteule Donald Trump ametaja msamaha wa Biden kwa mwanaye kuwa hujuma kwa haki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW