1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCape Verde

Biden atua kwa muda nchini Cape Verde akielekea Angola

2 Desemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ametua kwa muda nchini Cape Verde kabla ya kuendelea na safari yake kuelekea nchini Angola.

MArekani | Rais Biden aelekea Angola kwa ziara rasmi
Ziara ya Biden itajikita zaidi kwenye mradi mkubwa wa reli unaounganisha bandari ya Lobito ya Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na ZambiaPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Rais wa Marekani Joe Biden ametua kwa muda nchini Cape Verde kabla ya kuendelea na safari yake kuelekea nchini Angola atakapofanya ziara ya siku mbili.

Biden anayeondoka madarakani mwezi ujao, hakujibu maswali ya waandishi wa habari juu ya uamuzi wake wa kutoa msamaha wa rais kwa mwanae Hunter Biden, na hivyo kumkinga na uwezekano wa kufungwa jela kutokana na makosa ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria na kukwepa kulipa kodi.

Nchini Angola, Biden atakuwa na mkutano na Rais Joao Lourenco wa Angola na atatembelea makumbusho ya Kitaifa ya Utumwa katika mji mkuu Luanda.

Ziara yake itajikita zaidi kwenye mradi mkubwa wa reli unaounganisha bandari ya Lobito ya Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia zenye utajiri wa rasilimali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW