SiasaMarekani
Biden atumia hotuba ya hali ya taifa kuhimiza ushirikiano
8 Februari 2023Matangazo
Biden ameyasema hayo jana usiku wakati akitoa hotuba ya Hali ya Taifa iliyolenga kuihakikishia nchi ambayo imezingirwa na mashaka na kujawa na mgawanyiko wa kisiasa.
Wakati Biden, ambaye ana umri wa miaka 80, akijiandaa kwa kile kinachowezekana kuwa jaribio lake la pili la kutaka kuchaguliwa tena, alilenga kulithibitishia taifa lenye mashaka kuwa uongozi wake umeleta matunda ndani na nje ya nchi.