1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden azuru mradi wa reli nchini Angola, anapomalizia ziara

4 Desemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden anahitimisha ziara yake ya siku tatu kwa kuutembelea mradi mkubwa wa miundombinu ya reli unaofadhiliwa na nchi yake unaofahamika kama Ukanda wa Lobito.

Angola Luanda 2024 | Besuch Präsident Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa ziara yake ya Makumbusho ya Kitaifa ya Utumwa huko Luanda, Angola, Desemba 3, 2024.Picha: Elizabeth Frantz/REUTERS

Marekani na washirika wake wamewekeza katika ukarabati wa mradi huo mkubwa wa reli wa kilomita 1,300 unaoziunganisha Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Angola. Serikali yaBidenimesema mradi huo wa reli utasaidia kuimarisha maslahi ya kibiashara lakini pia kukabiliana na ushawishi wa China unaoimarika barani Afrika.Mradi huo unalenga kuendeleza ushawishi wa Marekani katika eneo hilo lenye utajiri wa madini ya kobalti, shaba na mengine muhimu yanayotumika kutengeneza betri, magari ya umeme na vifaa vya kielektroniki.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW