1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuvamiwa Bunge Marekani

6 Januari 2022

Rais wa Marekani, Joe Biden anajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu majengo ya bunge la Marekani yalipovamiwa, akiungana na wabunge.

Symbolbild USA Joe Biden am Telefon
Picha: White House/imago images/ZUMA Wire

Kukumbuka shambulio hilo la kikatili ambalo lililibadili kabisa bunge la nchi hiyo na kuibua wasiwasi ulimwenguni kuhusu mustakabali wa demokrasia ya Marekani. 

soma Polisi auawa kufuatia shambulizi Capitol Marekani

Katika kuadhimisha mwaka mmoja wa uvamizi wa bunge la Marekani, Capitol Hill, Biden na wabunge wa chama cha Democratic wataanzia leo Alhamisi katika ukumbi wenye sanamu za watu mashuhuri wa Marekani, moja ya maeneo ambayo watu waliovamia walikusanyika mwaka mmoja uliopita na kusitisha zoezi la kuhesabu kura. soma Wafuasi wa Trump wavamia bunge, dunia yaduwaa

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jen Psaki amesema Rais Biden anatarajiwa kuzungumzia ukweli wa kile kilichotokea, na kupambanua kati ya hilo na "uongo ambao wengi wamekuwa wakiueneza tangu muda huo," na kitendo cha kuendelea kukataa kuthibitisha kwa wanachama wengi wa Republican kuwa Biden alishinda uchaguzi wa mwaka 2020.

Warepublican kususia maadhimisho hayo

Picha: Brent Stirton/Getty Images

Shughuli kadhaa za maadhimisho ya leo yatahudhuriwa na wabunge wa chama cha Democratic, lakini takriban wabunge wa chama cha Republican wote kwenye bunge hilo, hawatohudhuria. Mgawanyiko huu ni ukumbusho mzito wa mpasuko kati ya pande hizo mbili, unaozidi kuwa mbaya tangu wakati huo mamia ya wafuasi wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump walipowavamia polisi, wakizua vurugu na kuvunja madirisha ya jengo la bunge na kusitisha shughuli za kuidhinisha ushindi wa Biden. Huku karibu wabunge wote wa chama cha Republican wakilaani mashambulizi hayo katika siku zilizofuata, wengi hata hivyo walibaki waaminifu kwa rais wao wa zamani.

soma Wademocrat watoa wito rasmi ili Trump aondolewe madarakani

Wakati wa kampeni ya mwaka 2020, Biden alisema msukumo wake wa kugombea kiti cha urais ilikuwa kupigania "nafasi ya taifa" baada ya kuona maoni ya Trump kwamba baadhi ya watu wema walikuwamo miongoni mwa watu weupe

wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia walioandamana huko Charlottesville, Virginia, mwaka wa 2017. Yeye alionya kuwa demokrasia ya Marekani iko hatarini, na maoni yake ni kwamba shambulio la Januari 6 lilikuwa dhihirisho la wazi la hofu yake.

Ushindi wa demokrasia

Rais Joe Biden na spika wa Bunge la Marekani Nancy PelosiPicha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi, anaadhimisha kumbukumbu hiyo akiliambia shirika la habari la The Associated Press katika mahojiano jana kwamba "demokrasia ilishinda usiku huo,'' wabunge waliporejea Capitol Hill baada ya ghasia na kuthibitisha ushindi wa Biden. Ili kuheshimu kumbukumbu hiyo, Pelosi amepanga muda wa ukimya katika bunge hilo.

soma Pelosi atoa idhini kutayarishwa mashtaka dhidi ya Trump

Ujumbe mkali wa Biden, ambao waRepublican wanajitenga nao, unatolewa huku wabunge wakizoea hali mpya na ya kawaida kwenye bunge la Marekani ambako mivutano inaongezeka na ambayo wengi wana wasiwasi itasababisha vurugu zaidi au, siku moja, uchaguzi ulio halali utatenguliwa. Wanachama wa Democratic na Republican wachache wanahisi haja kubwa ya kuungana na wananchi ambao baadhi wamekuwa wakiamini uongo wa Trump kwamba aliibiwa kura katika uchaguzi na kwamba shambulio hilo la majengo ya bunge la Marekani halikugubikwa na vurugu hata chembe.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW