1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden kuhakikishia Poland msaada huku hofu ikiongezeka Kyiv

12 Machi 2024

Rais wa Marekani Joe Biden leo anakutana na rais wa Poland Andrzej Duda na waziri mkuu Donald Tusk katika ikulu ya mjini Washington.

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzie wa Poland Andrzej Duda jijini Warsaw
Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzie wa Poland Andrzej Duda jijini WarsawPicha: JANEK SKARZYNSKI/AFP/Getty Images

Duda aliwahimiza washirika wa NATO kabla ziara hiyo kuongeza matumizi yao katika kuchukua hatua kushughulikia hofu inayoongozeka kuhusu uchokozi wa Urusi, na atamuomba Biden kupeleka wanajeshi zaidi wa Marekani kwa jumuiya ya NATO upande wa mashariki na Urusi.

Biden atajadili maadili ya demokrasia na viongozi hao wa Poland kufuatia hofu inayoongezeka ya kukosekana udhabiti wa kisiasa nchini mwao. Tusk amekuwa akilumbana karibu kila siku na rais Duda tangu aliposhinda uchaguzi Oktoba mwaka uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW