Biden kukutana na viongozi 18 wa Pasifiki Kusini
29 Aprili 2023Taarifa hiyo yenye kuonesha harakati mpya za Marekani za kustawisha mahusiano ya kikanda zimetolewa leo na wizara ya mambo ya nje ya taifa hilo.
Soma zaidi:Marekani yashauriwa kutoyapoteza mataifa ya pasifiki kwa China
Waziri wa Mambo ya Nje wa Papua New Guinea Justin Tkatchenko alisema Biden atahudhuria mazungumzo baina ya mataifa mawili na wenyeji wake na pia atakuwa na mkutano na viongozi 18 wa Visiwa vya Pasifiki kupitia Kongamano la Visiwa vya Pasifiki. Ukanda huo unaundwa na mataifa mengi madogo ambayo yametawanyika kote katika mwambao mkubwa wa bahari.
Marekani na China zipo katika jitihada za kuwania kupata ushawishi katika kile ambacho hapo awali kilikuwa kikiendeshwa kidiplomasia, ingawa sasa inazidi kuonekana kama nafasi muhimu kwa ushawishi wa kibiashara, kisiasa na kijeshi.