1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kukutana na Marcos na Kishida kuijadili China

11 Aprili 2024

Rais Joe Biden amemualika Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida katika Ikulu ya White House, kujaribu kuonyesha kuwa wamedhamiria kupambana na ushawishi wa kijeshi wa China

USA | Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden Picha: Paul Morigi/Getty Images for Care Can't Wait Action

Viongozi hao wanatarajiwa kutangaza kuwa walinzi wa pwani watafanya doria za pamoja katika eneo hilo la kusini mwa Asia mwaka huu. Hii inafuatia mazoezi ya pamoja yaliyofanywa na washirika hao karibu na eneo linalogombaniwa la Bahari ya China Kusini.

Mkutano huo wa kilele unajiri baada ya Biden kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Kishida katika hafla ya heshima ya kidiplomasia inayoashiria kuutambua ushawishi unaoongezeka wa Tokyo kwenye jukwaa la kimataifa.

China ilijibu kwa kusema kuwa Marekani na Japan zinaichafua na kuishambulia Beijing kuhusu masuala ya Taiwan na bahari ya China Kusini, zinaingilia masuala ya ndani ya China na kukiuka kabisa kanuni za msingi zinazosimamia ushirikiano wa kimataifa. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW