1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden kukutana na viongozi wa Ulaya Ijumaa

17 Oktoba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden atafanya ziara nchini Ujerumani Ijumaa ambapo atakutana na Kansela Olaf Scholz mjini Berlin.

Raius wa Marekani Joe Biden
Raius wa Marekani Joe BidenPicha: Ron Sachs/Pool/CNPZUMA Press Wire/IMAGO

Biden pia ameratibiwa kukutana na viongozi wengine wa Ulaya akiwemo Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer.

Ujerumani na Marekani wamekuwa wasaidizi wakubwa wa misaada ya kijeshi kwa Ukraine wakati inapopambana na uvamizi wa Urusi.

Lakini msemaji wa Ikulu ya White House, Karine Jean-Piere amesema kwamba Biden hatokutana na Rais Volodymyr Zelensky atakapokuwa Ujerumani.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, hatohudhuria mkutano huo wa Biden na viongozi wa Ulaya.

Meloni amesema Alhamisi kuwa hawezi kuuhudhuria mkutano huo kwa vyovyote vile kwani alikuwa amepanga ziara ya Mashariki ya Kati, ikiwemo ziara ya Lebanon.