Biden kukutana na Zelensky
11 Julai 2023Viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wamekusanyika katika mkutano wa kilele ambao utatawaliwa na ajenda ya vita nchini Ukraine pamoja na shinikizo la Kyiv la kutaka ikaribishwe haraka ndani ya jumuiya hiyo.
Soma zaidi: Erdogan aondoa pingamizi kwa Sweden kujiunga na NATO
Nchi wanachama wa NATO wanajadili jinsi ya kuondokana na mgawanyiko kuhusu jitihada za Ukraine kutaka uanachama huo, lakini wanadiplomasia kadhaa wamebainisha kuwa tofauti hizo zimepungua baada ya walio wengi kuafiki kuwa Ukraine haiwezi kujiunga na NATO wakati huu wa vita.
Soma zaidi: Biden awasili Uingereza kabla ya mkutano wa NATO
Wanachama wa NATO katika Ulaya Mashariki wanaunga mkono msimamo wa Kyiv, wakihoji kwamba kuijumuisha Ukraine chini ya mwamvuli wa usalama wa pamoja wa muungano huo wa kijeshi unaoongozwa na mataifa ya Magharibi ndio njia bora ya kuzuia Urusi kuishambulia tena.