1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden: Kuna uwezekano wa kukutana na Rais wa China

7 Oktoba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amesema hapo jana kuwa upo uwezekano wa kukutana na Rais wa China Xi Jinping mwezi ujao, pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki mjini San Francisco.

Indonesien Bali G20-Gipfel | Treffen Xi Jinping, Präsident China & Joe Biden, Präsident USA
Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Biden na Xi hawajazungumza tangu walipokutana mwezi Novemba mwaka jana katika mkutano wa kilele wa mataifa 20 yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi, G20 huko Bali, Indonesia. Maafisa wa serikali ya Marekani  wamekuwa wakijaribu kuwakutanisha viongozi hao huku Beijing ikitupilia mbali azma hiyo.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani umekabiliwa na mivutano ya kisiasa na kichumi. Tofauti kati ya nchi hizo mbili zimechochewa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine pamoja na harakati za China karibu na visiwa vinavyojitawala vya Taiwan.