SiasaMarekani
Biden: Majadiliano kuhusu deni la Marekani yamepiga hatua
20 Mei 2023Matangazo
Akizungumza kabla ya kukutana na viongozi wa kundi la mataifa manne linalofahamika kama QUAD pembezoni mwa mkutano wa G7 huko Hiroshima nchini Japan, Biden amesema hakuna sababu ya ulimwengu kuwa na wasiwasi juu ya deni la Marekani.
Amesema anaamini mazungumzo yanayoendelea kati yake na wabunge wa Republican yatazaa matunda, akipigia mfano kuwa duru ya pili na ya tatu ya mazungumzo hayo yamepata mafanikio fulani ya kutia moyo.
Serikali ya Biden inatanga kuongeza uwezo wake wa kukopa kufikia dola Trilioni 31.4 lakini wabunge kutoka chama cha Republican wanapinga mapendekezo hayo kwa hoja kwamba deni la nchi hiyo tayari limefikia kiwango cha kutia wasiwasi.