1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden na Modi wafanya mazungumzo juu ya vita nchini Ukraine

27 Agosti 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, siku chache tu baada ya kiongozi huyo wa India kuitembelea Ukraine.

Indien Ukraine | Indischer Premierminister Modi besucht Kiew
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akutana na Waziri Mkuu wa India Narendra ModiPicha: Gleb Garanich/REUTERS

Modi ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba amezungumza na Biden kuhusu "uungaji mkono kamili” wa India katika kurudisha amani na utulivu nchini Ukraine.

Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa inakaribisha jukumu la Modi kujaribu kurudisha amani nchini Ukraine.

Soma pia: Modi amrai Zelensky kukaa mezani kumaliza vita na Urusi

Msemaji wa baraza la usalama la kitaifa John Kirby amewaambia waandishi wa habari kuwa, Marekani inaunga mkono nchi yoyote inayojaribu kumsaidia Rais Volodymyr Zelensky kuelekea kupatikana kwa amani.

Ziara ya Modi mjini Kyiv imetokea baada ya kiongozi huyo wa India kukutana na Putin mjini Moscow mwezi uliopita.

Zelensky alimkosoa Modi kwa ziara yake mjini Moscow, iliofanyika siku moja wakati Urusi ilipofanya mashambulizi ya makombora nchini Ukraine na kusababisha vifo vya watu kadhaa.