Biden na Ruto kukutana mjini Washington
22 Mei 2024Ziara hiyo inafanyika katika wakati ambao taifa hilo likijitayarisha kuwapeleka askari wake nchini Haiti kama mpango unaoongozwa na Umoja wa Mataifa kujaribu kuyadhibiti magenge ya uhalifu yanayoongoza hujuma katika taifa hilo la Karibian.
Zaidi ya askari 1000 wa Kenya wanatazamiwa kuwasili Haiti hivi karibuni kama sehemu ya kikosi cha kimataifa cha kudhibiti magenge hayo ya uhalifu. Mataifa mengine yanayotarajiwa kuinga mkono Kenya ni Bahamas, Barbados, Benin, Chad na Bangladesh.
Kando na suala la Haiti, Juhudi za kujenga mahusiano ya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili pia zinatarajiwa kuwa ajenda ya mkutano wao.
Marekani kwa miaka mingi imekuwa ikishirikiana na Kenya katika juhudi za kupambanana ugaidi barani Afrika ikiwemo kupambana na kundi la Al Shabab.