1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na viongozi wa Ulaya wasisitiza ukomeshaji vita Gaza

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, na wote kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa kukomesha vita mara moja kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Emmanuel Macron, Joe Biden, Keir Starmer na Olaf Scholz mjini Berlin
Emmanuel Macron, Joe Biden, Keir Starmer na Olaf Scholz mjini BerlinPicha: Frederic Kern/Geisler-Fotopress/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, na wote kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa kukomesha vita mara moja kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza. Katika taarifa ya pamoja, viongozi hao walikubaliana juu ya kurejeshwa nyumbani haraka kwa mateka na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia raia.Rais wa Marekani Joe Biden amewasili mjini Berlin kwa ziara fupi

Aidha viongozi hao wanne walijadili kwa kina matukio ya Mashariki ya Kati, hususan athari za kifo cha kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar, ambaye anachukuliwa kuwa mratibu mkuu wa shambulio la kigaidi la Oktoba 7. Mbali na mzozo huo wa Mashariki ya Kati, pia wameahidi kuendelea kuisaidia Ukraine katika vita vyake na Urusi. Biden amefanya ziara yake fupi nchini Ujerumani wiki chache kabla ya uchaguzi wa Marekani.