1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na Xi kukutana Jumatano San Francisco

10 Novemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping wanatarajiwa kukutana Jumatano wiki ijayo eneo la San Francisco Bay, California nchini Marekani.

Rais wa China Xi Jinping  akiwa na mwenzake wa Marekani Joe Biden
Rais wa China Xi Jinping akiwa na mwenzake wa Marekani Joe BidenPicha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Kulingana na maafisa wa ngazi za juu wa Marekani, mkutano huo wa ana kwa ana utakaokuwa wa kwanza kati ya viongozi hao mwaka huu, unajiri kufuatia viwango vya juu vya diplomasia kwa lengo la kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili makubwa duniani.

Biden na Xi watakutana pembezoni mwa mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za kanda ya Asia na Pasifiki.

Maafisa wamesema mkutano huo utakaofanyika San Francisco unatarajiwa kujadili masuala yanayozonga ulimwengu ikiwemo vita vya Israel na Hamas, uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, uhusiano wa Korea Kaskazini na Urusi, Taiwan, kanda ya bahari ya Hindi na Pasifiki, masuala ya haki za binadamu, teknolojia ya akili ya kubuni na biashara.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW