1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na Zelensky wajadili mafunzo ya ndege za F-16

Sylvia Mwehozi
25 Agosti 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu mipango ya Washington ya kuwapatia mafunzo marubani wa Kiev kurusha ndege za kivita chapa F-16 katika vita vyake na Urusi.

F-16
Ndege ya kivita chapa F-16 Picha: Duncan C. Bevan/ZUMA Wire/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu mipango ya Washington ya kuwapatia mafunzo marubani wa Kiev kurusha ndege za kivita chapa F-16katika vita vyake na Urusi.

Ugiriki kuwafunza marubani wa Ukraine kurusha ndege za F-16

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani ya White House imesema kuwa viongozi hao wawili walijadili lini mafunzo hayo yataanza na idhini ya haraka ya Marekani kwa mataifa mengine kuipatia Ukraine ndege hizo baada ya kukamilika mafunzo.

Kulingana na wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, mafunzo hayo yataanza rasmi mwezi ujao. Kwa muda mrefu Ukraine imekuwa ikitafuta kupatiwa ndege hizo za kivita na za kisasa ili iweze kupambana na mashambulizi ya Urusi.

Uholanzi na Denmark kuipatia Ukraine ndege za kivita F-16

Washirika wa Marekani wa Ulaya tayari wametangaza kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kurusha ndege hizo za kivita zilizotengenezwa Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW