1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden: Nakipokeza kizazi kipya mwenge wa uongozi

25 Julai 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amesema "anapokeza mwenge kwa kizazi kipya" wakati akieleza sababu za kujiondoa kwake kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Rede an die Nation | US-Präsident Joe Biden
Picha: Evan Vucci/IMAGO/UPI Photo

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 ameeleza kuwa uamuzi wa kujiondoa kwenye mbio za urais ndio njia bora ya kuiunganisha Marekani.

Amewaahidi Wamarekani kwamba katika muda wa miezi sita ijayo, ataelekeza nguvu zake zote katika kuwahudumia.

Hayo ni sehemu tu yaliyomo kwenye hotuba yake iliyotolewa na Ikulu ya White House.

Hotuba ya leo ni yake ya kwanza kwa umma tangu alipotangaza Jumapili iliyopita kuwa hatowania tena urais kwa muhula wa pili.

Kiongozi huyo amekuwa akishinikizwa kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais na wanachama wenzake wa Democratic baada ya kufanya vibaya katika mdahalo wa urais dhidi ya mpinzani wake mgombea wa chama cha Republican Donald Trump.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW