1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden, Starmer kujadili silaha za masafa marefu kwa Ukraine

13 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amewasili mjini Washington, Marekani, ambapo atakutana na Rais Joe Biden kujadiliana ikiwa Ukraine inaweza kuruhusiwa kutumia makombora ya mashafa marefu dhidi ya Urusi.

USA | Uingereza | Keir Starmer na Joe Biden
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Marekani Joe Biden Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Ukraine inazishinikiza Marekani na Uingereza kuondoa vikwazo vya kuyatumia makombora ya masafa marefu yaliyotengenezwa na nchi hizo.

Urusi yashambulia kwa droni kaskazini mwa Ukraine

Hayo yanajiri mnamo wakati Rais Vladimir Putin wa Urusi akitahadharisha kwamba kuipa Ukraine ruhusa hiyo kutamaanisha Jumuiya ya Kujihami, NATO, ipo kwenye kwenye vita na Urusi.

Hapo jana, Starmer alisema mazungumzo hayo yatakuwa katika ngazi ya kimkakati kuhusu mzozo wa Ukraine na wa Mashariki ya Kati.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW