1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden: Ni lazima tuendeleze msaada wetu kwa Ukraine

18 Oktoba 2024

Rais Joe Biden wa Marekani ambae kwa hivi sasa yupo mjini Berlin, Ujerumani, tayari amekutana na mwenyeji wake, Rais Frank-Walter Steinmeier, katika Kasri la Bellevue mjini Berlin,

Berlin | Joe Biden na Frank-Walter Steinmeier
Rais Joe Biden akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier katika makazi ya Bellevue mjini Berlin, Ujerumani, Ijumaa, Oktoba 18, 2024.Picha: Matthias Schrader/picture alliance/AP

Baada ya kupokelewa na Rais Steinmeier, mapokezi ambayo yaliambatana na kwa gwaride la kijeshi Biden alitunukiwa tuzo ya juu zaidi ya Ujerumani, ijulikano kama "Grand Cross of the Order of Merit" mjini Berlin. Kwa kupokea tuzo hiyo, kiongozi huyo sasa anakuwa wa pili baada ya George H. W. Bush.

Katika kauli yake ya mwanzo katika ziara yake hiyo Biden amesema ni lazima wadumishe msaada wao kwa Ukraine, amemlaani Rais Putini kwa mashambilizi yake dhidi ya Ukraine na kusema NATO bado ipo madhubuti na pamoja kuliko huko nyuma.

Majadiliano kuhusu Urusi na Ukraine na Mashariki ya Kati

Lakini baadae kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81, atafanya mazungumzo yenye kuhusisha masuala ya mataifa mawili, lake na Ujerumani na Kansela, Olaf Scholz, ikiwa ni kabla ya mkutano wake na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer.

Rais Joe Biden akizungumza na wanahabari alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Brandenburg, Berlin, Ujerumani, Oktoba 17, 2024Picha: Elizabeth Frantz/REUTERS

Mazungumzo hayo huenda yakalenga zaidi vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati, ambayo yote yamekuwa na mabadiliko makubwa sana katika siku za hivi karibuni. Biden amewasili mji Berlin katika kipindi kifupi baada tangazo la Israel kwamba shambulizi lake limemuua kiongozi wa Hamas Yehya al-Sinwar, hatua wanayoitazama kama itatoa kutoa fursa ya kumalizika kwa mzozo wa mwaka mzima huko Gaza na kuachiwa huru mateka wa Israel waliosalia.

Soma zaidi:Biden kukutana na viongozi wa Ulaya Ijumaa

Kansela Scholz na Biden  pia wanatarajiwa kumjadili Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky  kile mwenye anachokiita "mpango wa ushindi" uliosubiriwa kwa muda mrefu, ambao aliutangaza juma hili katika kipindi ambacho pia kimegubikwa na hatua za kusonga mbele kijeshi za Urusi huko mashariki mwa Ukraine.

Katika pendekezo lake Rais Zelensky kuna hitaji la Ukraine kujumishwa haraka katika kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, pamoja na maombi ya ruhusa ya kutumia silaha za masafa marefu za Magharibi dhidi ya kuyalenga maeneo ya ndani zaidi katika ardhi ya Urusi, kwa lengo ya kuilazimisha serikali ya Moscow kufanya mazungumzo ya kumaliza vita.

Wasiwasi wa Ujerumani na Marekani katika mapambano dhidi ya Urusi

Mataifa ya Marekani na Ujerumani yamekuwa muhimu zaidi kwa Ukraine katika utoaji wa misaada ya kijeshi na kifedha, lakini Kansela Scholz na Rais Biden walipinga matakwa ya hivi karibuni ya Zelensky, wakihofia kuingizwa katika mapambano ya moja kwa moja na Urusi.

Ikumbukwe tu kwamba safari hii ya Bideninafanyika ikiwa ni takribani zaidi ya juma baada ya kughairi mipango yake ya awali ya kufanya safari ya hadi Ujerumani kutokana na Kimbunga Milton.

Chanzo DPA

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW