1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bila ya wanawake,habari haziwezi kuwa timamu

8 Machi 2013

Si wengi wanaoshangazwa kwamba wanawake hawawakilishwi vya kutosha katika sekta ya vyombo vya habari.Hata hivyo madhara ya hali hiyo ni makubwa,inasema Ripoti ya taasisi ya wakinamama katika vyombo vya habari-WMC

Wanawake katika maandalizi ya mijadala ya kisiasaPicha: AFP/Getty Images

Ripoti ya mwaka 2013 ya taasisi ya wakinamama katika vyombo vya habari WMC kuhusu hali ya wakinamama katika vyombo vya habari vya Marekani inashauri namna ya kuondokana na tofauti hizo hasa kwakua taasisi ya WMC yenyewe inalenga kubadilisha hali ya mambo katika sekta ya vyombo vya habari kupitia maudhui tofauti na madhubuti.

Ripoti hiyo imelengwa kuwa "wito wa kuizinduwa sekta ya vyombo vya habari na pia walimwengu kwamba wanachokiona,wakakisikia au kukisoma,hakijakamilika" amesema Julie Burton,ambae ni mwenyekiti wa taasisi ya WMC,katika mahojiano pamoja na shirika la habari la IPS na kuongezea "

Ikiwa utaratibu wa demokrasia utabidi kulindwa,WMC inaamini kwamba jamii inabidi ielewe uzito wa suala hili.Kutowakilishwa kwa hali ya usawa wakinamama katika nyanja za uandishi habari,filamu ,televisheni na radio kunapunguza juhudi za kuwapatia walimwengu picha halisi na tofauti ya hali ya mambo.

"Wanawake mara nyingi hawapatiwi fursa ya kukabidhiwa nafasi muhimu kama hizo kwasababu mambo kama hayo hukabidhiwa watu wenye madaraka-na kawaida ni wanaume ili wafanye kazi na wale wanaowajuwa." ameongeza kusema bibi Burton.

Wenye kudhibiti madaraka watakiwa wawajibike

Marie Colvin alikuwa akiripoti vitani,aliuliwa katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo februari 4 mwaka 2011Picha: picture alliance/dpa

Ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo taasisi ya WMC inafanya juhudi za kuondowa pengo lililoko la kijinsia kwa kuwapatia mafunzo wakinamama ili wawe tayari kujiunga na vyombo vya habari pamoja na kuandaa warsha ili kuwafanya wanaodhibiti madaraka wawajibike.

Katika mahojiano pamoja na ripota wa shirika la IPS, Julie Burton alizungumzia kuhusu changamoto zinazoikabili sekta ya vyombo vya habari katika mwaka 2013.Kuhusu uhusiano kati ya vyombo tofauti vya habari na namna ya kuimarisha demokrasia imara,bibi Burton amejibu kwa kusema:kwakuwa inajulikana kwamba idadi ya wanawake inapindukia nusu ya wakaazi wa dunia,ni jambo la kusikitisha kwamba katika vyombo vya habari,si wanawake wengi wanaoonekana au kusikika kama wenzao wa kiume.Kuna shida ya kuwawakilisha wanawake.Na hilo linaifanya sekta nzima ikose kuaminika."Vyombo vya habari na jamii inabidi iwakilishwe kikamilifu na sauti za kila upande pamoja na kutowa michango yao ili kuifanya demokrasia iwe imara zaidi.

Kuhusu suala kama wakinamama wanahimizwa wafuate fani ya uandishi habari baada ya kumaliza masomo yao,bibi Burton amejibu kwa kuelezea kile kilichodhihirika katika ripoti ya taasisi ya WMC kwa mwaka huu wa 2013;yaani wanawake wengi sasa wanavutiwa na kazi za uhusiano na umma au matangazo ya biashara.Lakini linapohusika na chumba cha habari changamoto inaendelea kuwa kubwa.Kupata kazi si suala linalohusiana na kipaji,mara nyingi linahusiana na unajuana na nani.Anasema bibi Burton na kusiosititza matumaini yao ni kuwaona wakinamama vijana wakiwa na moyo mkubwa zaidi na kuendelea kusaka njia za kujiunga na fani ya uandishi habari.

Njia bado ni ndefu

Mtangazaji nyota wa Marekani Optah WinfreyPicha: AP

Kuhusu suala kama anahisi jamii imejengeka ili kuamini zaidi kinachosemwa na watu wa jinsia ya kiume bibi Burton amejibu tunanukuu:"Wiki hii tunasherehekea kuchapishwa usimulizi unaoonyesha jinsi wakinamama walivyochangia katika kuibadilisha Marekani katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.Anasema wamepiga hatua muhimu mbele lakini pia anasisitiza kwamba njia iliyosalia ni ndefu.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/IPS

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi