1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BILD-ZEITUNG: Ujerumani wazidi Waislamu wa itikadi kali.

7 Desemba 2003
BERLIN: Kwa kulingana na vyombo vya habari, maafisa wa usalama wa Kijerumani wanazidi kutiwa wasi wasi na kule kuongezeka kiwango cha Waislamu wa itikadi kali nchini Ujerumani. Kwa kulingana na tathmini za mabingwa, Ujerumani wanaishi baina ya Waislamu 30,000 na 40,000 wa itikadi kali, liliandika gazeti la Kijerumani BILD AM SONNTAG. Kwa mujibu wa gazeti hilo, mwishoni mwa Novemba alikuwemo Muislamu wa Kijerumani mwenye itikadi kali mwenye miaka 25 miongoni mwa watu waliouawa nchini Chechenia. Shirika la Hifadhi ya Katiba ya Ujerumani linashutumu kuwa kijana huyo aliyeuawa alikuwa mwanachama wa chama cha Kipalestina JIHAD ISLAMIYYAH.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW