1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Bilionea Ratan Tata wa India afariki dunia akiwa na miaka 86

10 Oktoba 2024

Mkuu wa makampuni ya Tata Sons, N. Chandrasekaran, ametangaza kifo cha mwanzilishi wa makampuni hayo, bilionea Ratan Tata, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86 mjini Mumbai siku ya Jumatano (Oktoba 9).

Ratan Tata
Ratan Tata, aliyekuwa bilionea na mwanzilishi wa makampuni ya Tata Group.Picha: Sebasrtian Derungs/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu Narendra Modi alimuelezea Tata kama kiongozi mwenye maono na pia mtu aliyekuwa na kipaji kisicho cha kawaida.

Mkuu wa kampuni ya Google, Sundar Pichai, alisema Tata ameondoka duniani akiwacha alama kubwa ya mafanikio kwenye biashara na moyo wa ufadhili nchini India.

Soma zaidi: India: Makampuni yakabiliwa na mashambulizi ya mtandaoni

Tata Group ni mkusanyiko wa kampuni zaidi ya 100, ikiwemo kampuni kubwa ya kutengeneza magari nchini India.

Mwaka 1932 alikuwa mmojawapo wa waliojitolea kuanzisha wa kampuni ya ndege ya India, Air India, ambayo baadaye aliinunuwa rasmi mwaka 2021.