1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bingwa wa riadha Kenya Kelvin Kiptum afariki kwa ajali

12 Februari 2024

Ulimwengu wa riadha bado unaomboleza kifo cha mwanaridhiadha anayeshikilia rekodi ya dunia, Kelvin Kiptum kutoka Kenya, aliyefariki jana kutokana na ajali ya barabarani.

Mwanariadha Kelvin Kiptum afariki dunia
Kelvin Kiptum enzi za uhai wakePicha: Alberto Pezzali/AP Photo/picture alliance

Mwanaridhia huyo alipata ajali kwenye eneo la bonde la Ufa baada ya kushindwa kulidhibiti gari alilokuwa akiendesha na kuacha barabara.Jackson Tuwei, rais wa chama cha riadha nchini Kenya amesema Kiptum alikufa hapo hapo baada ya ajali hiyo.

"Katika ajali hiyo Kelvin alipoteza mwekeo na kushindwa kulidhibiti gari  na kutoka nje ya barabara  kisha kuingia kwenye shimo.Alilidhibiti  gari akiliendesha kwa  mita sitini kabla ya kugonga mti mkubwa. Na naamini hicho ndicho kilichosababisha madhara haya tunayoizungumzia."

Soma pia: Kiptum atahadharishwa baada ya kuvunja rekodi ya dunia

Rais wa chama cha riadha duniani Sebastian Coe kupitia taarifa yake amesema wameshtushwa na kuhuzunishwa sana na kifo cha Kelvin Kiptum pamoja na kocha wake, raia wa Rwanda Gervais Hakizimana. Ametowa salamu za rambi rambi akisema wamempoteza mwanariadha mahiri aliyeacha sifa kubwa.

Kelvin Kiptum aliyekuwa na umri wa miaka 24 aliweka rekodi ya dunia katika mashindano ya riadha ya mbio za Marathon, Chicago mwezi Oktoba kwa kukimbia kwa muda wa saa mbili na sekunde 35 na kuvunja rekodi iliyowekwa na Eliud Kipchoge mjini Berlin mwaka 2022 ya kukimbia kwa saa mbili, dakika moja na sekunde tisa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW