1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BioNTech kufanya majaribio chanjo ya Malaria

23 Desemba 2022

Kampuni ya madawa ya Ujerumani ya BionTech imeanza kufanya majaribio ya chanjo ya malaria.

Deutschland | Coronaimpfung Biontech
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kampuni hiyo imesema leo kuwa inafanya majaribio ya usalama na ufanisi wa chanjo hiyo inayoitwa BNT165b1, katika awamu ya kwanza.

Watu watakaofanyiwa majarabio hayo wataangaliwa katika viwango vitatu tofauti vya dozi.

Ozlem Tureci, mwanzilishi mwenza wa BionTech amesema kuanzishwa kwa majaribio haya ni hatua muhimu katika juhudi zao za kusaidia kukabiliana na magonjwa yenye uhitaji mkubwa wa matibabu.

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO, takribani watu 619,000 walikufa duniani kwa kuugua malaria mwaka 2021, ikiwa ni idadi pungufu ya watu 625,000 mwaka uliotangulia.

Asilimia 95 ya watu wanaougua malaria na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vilitokea barani Afrika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW