1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bisau. Ghasia nchini Guinea Bisau zasababisha polisi wawili kuuwawa.

17 Julai 2005

Ghasia katika taifa la Afrika magharibi la Guinea Bisau zimesababisha polisi wawili kuuwawa na wengine kumi wamejeruhiwa.

Maafisa wamesema kuwa makao makuu ya rais na wizara ya mambo ya ndani yalishambuliwa na watu hao wenye silaha.

Polisi wamewakamata watu 20 waliohusika katika shambulio hilo. Sababu za ghasia hizo, ambazo zimekuja wiki moja kabla ya duru ya pili na ya mwisho ya uchaguzi wa rais, hazikujulikana mara moja. Majeshi ya nchi hiyo yamesema kuwa hali hiyo sasa imekwisha dhibitiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW