1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISHKEK: Issabekov ajiuzulu kuhifadhi utulivu Kyrgyzstan

29 Machi 2007

Waziri mkuu wa Kyrgyzstan Asim Issabekow amejiuzulu.Amesema amechukua hatua hiyo kuhifadhi hali ya utulivu nchini humo.Msemaji wa serikali katika mji mkuu Bishkek amesema,Rais Kurmanbek Bakiyev amemteua kiongozi wa upinzani Almas Atambayew kuiongoza serikali kwa muda.Issabekow alishika madaraka mwisho wa mwezi Januari,baada ya bunge kushindwa kumrejesha madarakani kiongozi wa zamani Felix Kulow.