BISHTEK : Steinmeir akamilisha ziara Asia ya Kati
5 Novemba 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir ametowa wito wa kuwepo Umoja wa Ulaya wenye nguvu katika majimbo matano ya zamani ya Muungano wa Urusi yenye utajiri wa rasilmali.
Steinmeir alifanya ziara ya wiki moja katika nchi hizo kwa kuanzia na Kazakhstan na kukamilisha ziara yake kwenye nchi iliokosa utulivu ya Kyrgystan baada ya kuitembelea Uzbekistan.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema kwamba kuwa na sera kwa ajili ya eneo hilo yatakuwa miongoni mwa mambo ya kupewa kipau mbele wakati Ujerumani itakaposhika wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya wa nchi wanachama 25 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2007.