1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISSAU: Mivutano kabla ya uchaguzi nchini Guinea Bissau

17 Mei 2005

Kiongozi wa kundi la wakuu wa kijeshi,lenye ushawishi mkubwa nchini Guinea Bissau,ameahidi kumuunga mkono rais wa mpito wa nchi hiyo. Jemadari Bitchofela Na Fafe,ambae ni mkuu wa kamati ya kijeshi iliyompindua Yalla mwaka 2003,amewaambia maripota kuwa kamati hiyo inamuunga mkono rasi wa mpito Henrique Rosa.Ahadi hiyo imetolewa siku moja baada ya Kumba Yalla aliepinduliwa kusema kuwa yeye ndie kiongozi halali wa nchi.Kwa sababu ya tangazo hilo,kuna wasi wasi kwamba mivutano itazuka katika koloni la zamani la Mreno,kabla ya uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanywa mwezi ujao.Kamati ya kijeshi inayoishauri serikali,hasa ina majemadari wa kabila la Balante sawa na Yalla.Inadhaniwa kuwa baadhi ya majemadari hao sasa wanamuunga mkono tena Yalla,ingawa miaka miwili ya nyuma walichangia kumpindua.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW