1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blair, Rubio watajwa katika orodha ya 'Bodi ya Gaza'

17 Januari 2026

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, atakuwa miongoni mwa wajumbe wa “Bodi ya Amani ya Gaza” ya Rais wa Marekani Donald Trump, ambayo inalenga kuzuia migogoro ya baadaye katika eneo hilo.

Misri Sharm El Sheikh 2025 | Tony Blair na Donald Trump katika Mkutano unaohusu Gaza
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair(kushoto) na Rais Donald Trump Oktoba 2025Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, atakuwa miongoni mwa wajumbe wa "Bodi ya Amani ya Gaza” ya Rais wa Marekani Donald Trump, ambayo inalenga kuzuia migogoro ya baadaye katika eneo hilo.

Jina la Blair limeorodheshwa pamoja na maafisa wengine waandamizi katika utawala wa Trump kama sehemu ya baraza kuu la waanzilishi,  litakaloongoza juhudi za muda mrefu za kuleta amani katika kanda ya Mashariki ya Kati, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani White House.

Orodha hiyo pia inamjumuisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, mjumbe maalum wa Mashariki ya Kati Steve Witkoff, na mkwe wa Trump Jared Kushner.

Wajumbe wengine waliotajwa ni bilionea Marc Rowan, rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga, na naibu mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Robert Gabriel.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW