Blatter azilaumu Ufaransa na Ujerumani
6 Julai 2015Matangazo
Rais wa shirikisho la soka Duniani, FIFA, Sepp Blatter ameishutumu Ufaransa na Ujerumani kuwa zilitumia shinikizo za kisiasa, kutaka Urusi na Qatar kuchaguliwa kuwa wenyeji wa kombe la dunia, 2018 na 2022.
Akizungumza na gazeti la Ujerumani - Welt am Sonntag, Blatter, alidai kuwa rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, na mwenzake wa Ujerumani, Christian Wulff, walijaribu kuwashawishi wawakilishi wa nchi zao, kabla ya kupigwa kura za kutolewa vibali vya wenyeji wa Kombe la Dunia
Blatter, ambaye sasa anachunguzwa na shirika la upelelezi la Marekani -FBI, kuhusu tuhuma za rushwa, amesema amechoka kubeba lawama kwa jambo ambalo halikuwa mikononi mwake .
Mwandishi: Bruce Amani/Reuters
Mhariri: Josephat Charo