Blinken aelekea Brussels kwa mazungumzo kuhusu Ukraine
12 Novemba 2024Matangazo
Katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu Trump alipochaguliwa tena, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ataizuru Brussels kabla ya kuelekea Peru na Brasil baadae wiki hii.
Vikosi vya Ukraine vyakabiliana na askari 50,000 wa Urusi katika mkoa wa Kursk
Katika mikutano na viongozi wa jumuiya ya kujihami ya NATO na Umoja wa Ulaya, Blinken atajadili uungaji mkono kwa Ukraine katika ulinzi wake dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Trump amekuwa mkosoaji wa msaada wa Biden kwa Ukraine na hivyo kuzusha mashaka ya kwamba huenda akaacha kuiunga mkono serikali ya Volodymyr Zelensky.