1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Blinken na Starmer kujadili namna ya kuisaidia Ukraine

10 Septemba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema atajadilana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na maafisa wengine kuhusu juhudi za kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameenda Uingereza kuzungumzia mizozo ya Gaza na UkrainePicha: Roberto Schmidt/Pool photo via AP/picture alliance

Katika mkutano huo utakaofanyika London, viongozi hao watajadili pia kuhusu namna ya kukabiliana na mzozo wa Mashariki ya Kati.

Kulingana na wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Blinken atajadiliana pia na Waziri Mkuu Stammer na Waziri wa Mambo ya Kigeni David Lammy kuhusu ukanda wa Indo-Pasifiki na mkataba wa ulinzi wa AUKUS kati ya Marekani, Australia na Uingereza.

Ziara ya Blinken nchini Uingereza inafanyika baada ya afisa wa juu wa Iran kukanusha ripoti kuwa Tehran iliipa Urusi makombora ya masafa  marefu, Umoja wa Ulaya ukisema taarifa hiyo ni ya kuaminika.