1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Blinken afanya ziara nchini Iraq kuhusu hali ya Syria

13 Desemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na waziri mkuu wa Iraq Mohammed Shia al-Sudani.

Mohammed Shia al-Sudani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq
Mohammed Shia al-Sudani, Waziri wa Mambo ya Nje wa IraqPicha: Thaier Al-Sudani/REUTERS

Blinken amefanya ziara hiyo ya kushtukiza akijaribu kuratibu mikakati ya kikanda kuhusu mustakabali wa Syria kufuatia kupinduliwa kwa rais Bashar al-Assad.

Blinken na al-Sudani watajadili masuala ya ushirikiano na changamoto za usalama wa kikanda, pamoja na mchango wa Marekani katika kufanikisha kipindi cha mpito shirikishi nchini Syria.

Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Marekani amewasili Baghdad akitokea mji mkuu wa Uturuki Ankara alipokutana pia na Rais Tayyip Erdogan ambaye walijadili pia suala hilo na kumueleza umuhimu wa kuwalinda raia wa Syria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW