1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken aitaka Mashariki ya Kati kujizuia kuongeza mzozo

1 Agosti 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amezitolea wito pande zinazovutana Mashariki ya Kati kujizuia na hatua zitakazochochea mzozo na kukubaliana kusitisha mapigano, Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Blinken
Blinken amezitolea wito pande zinazovutana Mashariki ya Kati kujizuia na hatua zitakazochochea mzozoPicha: TED ALJIBE/AFP

Akizungumza katika mji mkuu wa Mongolia, Blinken alionya kwa kusema Mashariki ya Kati inaelekea kwenye mzozo zaidi, machafuko, mateso na kukosekana usalama, na kuongeza kuwa ni muhimu mzunguko huu ukavunjwa.

"Antony Blinken: Na ili kufika hapo, kwanza inatakiwa pande zote kuachana na matukio ya uchochezi. Pia wanatakiwa kusaka sababu ya kukubaliana, na si sababu ya kuchelewesha ama kuyakataa makubaliano. Na ni muhimu kwamba pande zote zifanye maamuzi sahihi katika siku zijazo."

Soma pia: Baraza la Usalama la UN laijadili hali ya Mashariki ya Kati

Kifo cha kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh kilichotokea masaa kadhaa baada ya Israel kusema imemuua kamanda wa juu wa Hezbollah, vinachukuliwa kuuchochea mzozo katikati ya wasiwasi mkubwa unaozidishwa na vita vya Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW