SiasaIsrael
Blinken akutana na Abbas mjini Amman
13 Oktoba 2023Matangazo
Blinken pia amekutana na Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan, ambaye ametahadharisha juu ya kuwahamisha Wapalestina huku Israel ikiandaa harakati kubwa ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza.
Mfalme Abdullah wa pili amesema mzozo huo hautakiwi kuenea katika nchi jirani na kuzidisha tatizo la wakimbizi.
Blinken aliwasili Jordan jana jioni akitokea Israel na atakwenda pia Qatar, Saudi Arabia, Misri na Umoja wa Falme za kiarabu wakati Marekani ikipania kuongeza shinikizo dhidi ya kundi la Hamas.