1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Antony Blinken kuzuru Afrika

19 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, mwishoni mwa juma hili anatarajiwa kuanza ziara yake barani Afrika.

Misri | Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Cairo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipokuwa akiwasili nchini Misri Januari 11, 2024 kwa ziara iliyolenga kupunguza wasiwasi katika Mashariki ya KatiPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Blinken atayatembelea mataifa ya Cape Verde, Ivory Coast, Nigeria na Angola kuanzia Januari 21 katika ziara itakayomalizika Januari 26.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema akiwa barani Afrika, Blinken atajadili ushirika wa Marekani na Afrika katika masuala ya biashara, hali ya hewa, miundombinu na afya.

Masuala mengine yatakayoangaziwa ni pamoja na usalama wa kikanda, kuzuia mizozo na kukuza demokrasia.

Msaidizi wa Blinken anayeshughulikia masuala ya Afrika, Molly Phee amesema kuwa ziara ya Blinken barani Afrika ni sehemu ya ufuatiliaji wa mkutano uliofanyika Washington na kuhudhuriwa na viongozi wa bara hilo mwaka 2022 ambapo Rais Joe Biden aliahidi kuwa Marekani iko kwa ajili ya mustakabali wa Afrika.