1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Blinken awasili Uturuki kuanza ziara Mashariki ya Kati

6 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken amewasili nchini Uturuki jana Ijumaa kuanza ziara ya siku nne huko Mashariki ya Kati, tangu kulipoibuka mzozo kati ya Israel na Hamas miezi mitatu iliyopita.

India | Antony Blinken katika mkutano wa kundi la G20
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kando ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20, Alhamisi, Machi 2, 2023, mjini New Delhi. Blinken yuko Mashariki ya Kati kwa ziara ya siku nne. Picha: Olivier Douliery/AP Photo/picture alliance

Blinken atazuru Israel, na mataifa mengine matano ya Kiarabu ya Misri, Jordan, Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, imesema wizara ya mambo ya nje.

Blinken hii leo atafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye ni mmoja ya mkosoaji mkubwa kutoka kwenye ulimwengu wa Kiislamu juu ya namna Marekani inavyoiunga mkono Israel kwenye mzozo huo.

Blinken alitumia ziara za huko nyuma kujaribu kuzuia vita kusambaa, lakini sasa anarejea kwenye ukanda huo ambao umeshuhudia mashambulizi kutokea ama kuelekea Lebanon, Iraq, Yemen, Syria na Iran.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi