1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken asema Israel inahitaji kuisaidia Palestina

17 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameitaka Israel kuisaidia badala ya kuizuia mamlaka ya Palestina, akisema usalama wa muda mrefu wa Israel uko hatarini.

Israel Jerusalem | Antony Blinken na Benjamin Netanjahu
Waziri wa masuala ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Ronaldo Schemidt via REUTERS

Blinken amerudia wito wake wa kuwepo "njia ya kuelekea kupatikana kwa taifa la Palestina" licha ya Marekani kuiunga mkono Israel katika vita vyake dhidi ya kundi la Hamas.

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani ameongeza kuwa, mamlaka ya Palestina inaweza tu kuwa na ufanisi iwapo itafanya kazi kwa ushirikiano wa Israel na wala sio upinzani.

"Unazungumza juu ya utawala, serikali na muundo wa utawala, ambao utaiwezesha mamlaka ya Palestina kuwapa mahitaji raia wa Palestina. Kwa hivyo, mamlaka hiyo inapaswa iwe inafanya kazi katika mazingira mazuri, kwa maneno mengine, isaidiwe na Israel na wala sio kukabiliwa na upinzani, alisema Blinken"

Msaada zaidi wa kibinaadamu kuwasili Gaza


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa muda mrefu ameonyesha upinzani kwa mamlaka ya Palestina na uwepo wa taifa huru la Palestina.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW