1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Blinken ataka suluhisho la kidiplomasia Mashariki ya Kati

12 Juni 2024

Antony Blinken kwa mara nyengine Jumatano ametoa wito wa suluhisho la kidiplomasia kati ya Israel na Lebanon na kusema kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza, yatasaidia pakubwa kupunguza mivutano.

Antony Blinken akiwa mjini Doha, Qatar
Antony Blinken akiwa mjini Doha, QatarPicha: Ibraheem Al Omari/AP/picture alliance

Blinken ameyasema hayo mwishoni mwa ziara yake ya Mashariki ya Kati ambapo alikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye ametoa kauli kali kulihusu kundi la Hezbollah nchini Lebanon.

Blinken amesema suluhisho lolote linahitajika ili kuhakikisha kwamba watu wanarudi majumbani kwao kaskazini mwa Israel na kusini mwa Lebanon.

Wanamgambo hao wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran, wamefanya mashambulizi ya maroketi kaskazini mwa Israel Jumatano baada ya shambulizi la Israel kusababisha kifo cha kamanda mmoja mkuu.