1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken yuko Misri kwa ajili ya Israeli na Palestina

26 Mei 2021

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewasili nchini Misri leo kwa ziara ya kushinikiza juhudi za kusitisha mapigano kati ya Israeli na wapiganaji wa Palestina huko Gaza.

Israel Jerusalem | US Außenminister Blinken
Picha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Blinken amewasili nchini Misri Jumatano katika awamu ya pili ya ujumbe wake wa kidiplomasia unaolenga kudumisha makubaliano ya kusitisha mapigano yaliomaliza vita vya siku 11 kati ya Israel na kundi la wapiganaji la Hamas..

Blinken anatarajiwa kukutana na rais wa nchi hiyo Abdel Fattah-el Sissina maafisawengine wakuu katika serikali ya nchi hiyo.

Wakati wa ghasia kati ya Israeli na Paestina, Biden alizungumza na el-Sissi kusaidia kuafikia mkataba wa kusitisha mapigano. Blinken ameweka malengo ya kawaida kwa ziara hiyo ambayo ni ya kwanza rasmi kwa Mashariki ya Kati kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Yaliojiri wakati wa mkutano wa Blinken, Abbas na Rivlin

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani tayari ashakutana na viongozi wa Israeli na Palestina kuonesha kujitolea kwa Marekani katika kuunga mkono makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa siku ya Ijumaa ambayo yalimaliza mashambulizi ya siku 11 ya mabomu yaliyofanywa na Israeli katika ukanda wa Gaza na urushaji wa maroketi ya moto kutoka eneo hilo kuelekea Israeli.

Baada ya mazungumzo na rais wa Palestina Mahmud Abbas katika makao yake makuu katika ukingo wa Magharibi, Blinken aliahidi kujenga upya uhusiano wa Marekani na Wapalestina kwa kufungua tena ubalozi mdogo nchini humo pamoja na kutoa mamilioni kupitia msaada katika eneo ukanda wa Gaza.

Kabla ya kuondoka nchini Israeli, Blinken aliwasilisha mualiko wa rais Joe Biden kwa rais wa nchi hiyo Reuven Rivlin kuzuru Marekani katika wiki zijazo. Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais huyo inasema kuwa rais Rivlin alikubali mualiko huo.

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin

Huku hayo yakijiri, wakati wa mkutano wa kilele wa Juni 16 mjini Geneva, agenda yake inatarajiwa kujumuisha mazungumzo kuhusu hatua za Urusi katika taifa jirani la Ukraine, kugeuzwa kwa safari ya ndege iliyokuwa ikielekea Lithuania hatua iliyochukuliwa na mshirika wa Urusi, Belarus pamoja na juhudi za mataifa yote ya kukabiliana na virusi vya corona.

Matarajio ya mkutano huo

Ni katika mkutano huu ambapo rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Urusi wa Vladmir Putin wamekubaliana kukutana ana kwa ana. Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jen Psaki amesema kuwa hakuna masharti yaliyowekewa mkutano huo na kwamba matarajio ya ikulu hiyo yako chini.

Badala yake, maafisa wa serikali wanasema kuwa mwanzoni wa kipindi chake kama rais, Biden alikuwa ameonya kuwa anatarajia uhusiano kati ya Marekani na Urusi utaendelea kuwa wa utata lakini sasa anatafuta kuafikia makubaliano na taifa hilo kuhusu mustakabali wa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa upande wake, ikulu ya Kremlin imesema kuwa marais hao wawili watazungumzia hali ilivyo sasa na uwezekano wa uhusiano kati ya Marekani na Urusi, masuala ya uthabiti wa kimkakati na masuala tete katika agenda ya kimataifa yanayojumuisha ushirikiano katika kukabiliana na janga la virusi vya corona na pia kusuluhisha migogoro ya kikanda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW