1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Blinken azungumza na Bazoum kwa njia ya simu

Josephat Charo
10 Oktoba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amezungumza kwa njia ya simu na rais wa Niger aliyeondolewa mamlakani Mohamed Bazoum.

Rais wa Niger aliyeondolewa mamlakani Mohamed Bazoum.
Rais wa Niger aliyeondolewa mamlakani Mohamed Bazoum.Picha: Stevens Tomas/ABACA/IMAGO

Mazungumzo hayo yamejiri kabla ya uamuzi unaotarajiwa kuchukuliwa na utawala wa rais Joe Biden kutangaza rasmi kwamba kuondolewa kwake madarakani yalikuwa mapinduzi.

Wizara ya mambo ya ndani imesema Blinken alimpigia simu Bazoum kusisitiza kwamba kurejeshwa kwa serikali iliyochaguliwa kwa uhuru ndio njia muafaka kwa Niger kustawi kwa ajili ya watu wake.

Imeongeza pia kuwa hiyo ndiyo njia itakayohakikisha nchi hiyo inaendelea kuwa mshirika muhimu wa Marekani na nchi nyingine katika vita dhidi ya misimamo mikali na ugaidi katika eneo la Sahel.

Wizara hiyo imesema Marekani inataka watu wote wanaozuiliwa kwa njia isiyo halali baada ya jeshi kutwaa madaraka waachiwe huru mara moja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW