1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken azungumza na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi

30 Januari 2023

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mjini Cairo leo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu kwenye kanda ya Mashariki ya Kati

Ägypten | Antony Blinken zu Besuch in Kairo
Picha: U.S. Department of State/Anadolu Agency/picture alliance

Bw Blinken amekutana na rais Al-Sisi pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Misri Sameh Shoukry kwa majadiliano ya masuala ya kikanda ikiwemo juhudi za kumaliza mzozo nchini Sudanna kukomesha mapigano baina ya pande hasimu nchini Libya.

Soma pia:Blinken: Marekani kutoa tangazo 'zito' kuiunga mkono Afrika

Baadaye ataelekea mjini Jerusalem kwa mkutano na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netayahu ambaye sera za serikali yake zimezusha wasiwasi mkubwa wa kuongeza mivutano kwenye kanda hiyo.

Waziri Blinken atasafiri pia hadi mjini Ramallahhuko Ukingo wa Magharibi kwa mazungumzo na kiongozi wa mamlaka ya ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas.