Blinken: Iran inaendelea na uundaji wa silaha za nyuklia
20 Julai 2024Matangazo
Habari hizo kuhusu uwezo wa Iran zinatolewa baada ya uchaguzi wa hivi karibuni uliomuingiza madarakani Rais Masoud Pezeshkian, ambae alisema lengo lake ni kuiondoa Iran katika hali ya kutengwa, na kuonesha nia ya kufufua mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani.
Blinken anasema kile wanachokishuhudia wiki iliyopita na miezi kadhaa nikitendocha Iran kuendelea na mpango wake wa nyuklia.
Mwaka 2018, Marekani ilijiondoa katika mpango wa nyuklia, ambao uliundwa katika namna ya kudhibiti mwenendo wa matumizi ya nishati ya atomik wa Iran, kwa makubaliano ya jumuiya ya kimataifa kuliondolewa taifa hilo vikwazo.