1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken kufanya ziara nyingine Mashariki ya Kati

21 Oktoba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa hivi karibuni kufanya ziara nyingine huko Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: TANG CHHIN SOTHY/via REUTERS

Hayo yameelezwa hapo jana na Makamu wa rais Kamala Harris ambaye amesisitiza kuwa nia yao ni kuvimaliza vita katika eneo hilo. Harris ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama cha Democratic amesema idadi ya  Wapalestina wasio na hatia ambao wameuawa huko Gaza haikubaliki.

Wizara afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas imesema watu zaidi ya 42,000 wameuawa. Israel imeendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza na nchini Lebanon, huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisema kuwa kundi la Hezbollah litalipa kwa gharama kubwa kitendo cha kudhamiria kumuua baada ya makazi yake kushambuliwa kwa droni katika mji wa Caesarea.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW